Sura ya Tatu: Kuipenda na Kujivunia Nchi Yako (Uraia na Maadili)
Document Details
Uploaded by InviolableSard3609
null
Tags
Summary
This Swahili document is about citizenship and values, focusing on appreciating and being proud of one's country. It discusses the importance of peace, law, and international relations within a community. It has a clear structure with categorized sections and a potential use in a Swahili-medium secondary-school setting in East Africa.
Full Transcript
FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Tatu Kuipenda na kujivunia nchi yako Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza ujumbe uliomo katika kaulimbiu na wimbo...
FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Tatu Kuipenda na kujivunia nchi yako Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza ujumbe uliomo katika kaulimbiu na wimbo wa shule, matendo yanayoiletea sifa shule na njia za kuitangaza shule yako. LY Pia, ulijifunza kuipenda, kuitangaza na kubaini njia mbalimbali za kuitangaza nchi yako. Katika sura hii, utajifunza jinsi ya kushiriki katika kuhamasisha na kudumisha amani katika jamii yako. Aidha, utaweza kushiriki katika vitendo N vya kulinda uhuru na umoja wa Taifa letu la Tanzania na kutenda vitendo vya O kuthamini utu katika jamii. Maarifa na ujuzi utakaopata utakuwezesha kuwa mzalendo kwa nchi yako. Fikiri SE U Hali inavyokuwa katika nchi isiyokuwa na amani. Kudumisha amani katika jamii E Amani ni hali ya utulivu na usalama, isiyokuwa na ghasia, fujo au vita. Amani katika jamii huweka misingi imara ya kulinda usalama wa raia na mali zao N na kudumisha utulivu kwa kuepuka ghasia, fujo au vita. Ili kudumisha amani, wananchi hawana budi kutii sheria, kulinda mipaka ya nchi, kuheshimu haki LI za binadamu, kukemea vitendo viovu, na kujenga uhusiano mwema na watu N na mataifa mengine. O Kutii sheria ni kuheshimu kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka zinazohusika bila kulazimishwa. Utii wa sheria husaidia kudumisha amani kwa sababu unaondoa migogoro na misuguano miongoni mwa wananchi au R kati ya wananchi na Serikali. Hivyo, sheria zimewekwa ili kuongoza matendo FO ya watu katika maisha yao ya kila siku. Ulinzi wa mipaka ya nchi yetu ni jukumu la kila mwananchi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Kila mwananchi analo jukumu la kutoa taarifa 24 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 24 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY kwa vyombo vya dola DO NOT endapo DUPLICATE ataona vitendo vinavyohatarisha usalama wa mipaka ya nchi. Baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na utoroshaji wa rasilimali za nchi kupitia mipaka ya nchi, uingizaji wa raia wa nchi zingine bila kufuata utaratibu, na biashara za magendo mipakani. Amani katika jamii inaweza kudumishwa kwa kuheshimu haki za msingi za binadamu kama vile, haki ya kuishi na kupata mahitaji muhimu kama chakula, malazi, mavazi, elimu, ulinzi na usalama wa mtu na mali zake. Pia, haki nyingine za msingi ni kushiriki katika mambo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. LY Vilevile, amani na usalama wa nchi yetu unaweza kudumishwa kwa kuhakikisha kuwa kuna uhusiano mwema kati ya nchi yetu na mataifa N mengine. Uhusiano mwema na nchi jirani huanza kwa wananchi wanaoishi O mpakani mwa nchi zinazohusika kutii sheria na taratibu za kila nchi. Uhusiano mwema na nchi nyingine huwezesha kuepuka migogoro, ugomvi na vita. Hali hii itawezesha nchi yetu kudumisha amani na usalama. SE Katika kila jamii kuna watu ambao huwa na mwelekeo hasi katika kudumisha amani. Kwa mfano, kuwapo kwa watu wachache wanaovunja sheria kama U vile, kufanya vitendo vya wizi na ubadhirifu. Hivyo, jamii haina budi kukemea mwenendo huu mbaya ili usiathiri amani na usalama wa jamii na nchi kwa ujumla. E Njia za kuhamasisha jamii kudumisha amani N Amani ni moja ya tunu adhimu za Taifa letu. Kuna njia mbalimbali za LI kuhamasisha jamii kudumisha amani ikiwa ni pamoja na kutumia kazi za sanaa, michezo, mitandao ya kijamii, siku ya amani, mahubiri na mihadhara N ya dini. Kwa kutumia njia hizi, ujumbe kuhusu umuhimu wa amani na madhara ya kutokuwa na amani huwafikia watu kwa urahisi. O Ngonjera, mashairi na michezo ya kuigiza hutumiwa katika kuelimisha umma kupitia matamasha mbalimbali hasa wakati wa sikukuu za kitaifa R kama vile, tarehe 9 Disemba, ambayo ni Sikukuu ya Uhuru; tarehe 26 FO Aprili, ambayo ni Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; au tarehe 12, Januari ambayo ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, tarehe 1 Mei, ambayo ni Sikukuu ya Wafanyakazi; na tarehe 8 Agosti, ambayo ni Sikukuu ya Wakulima. Sikukuu hizi zinaweza kutumika kama majukwaa ya 25 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 25 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY kuhamasisha jamii kulindaDO NOT amani DUPLICATE kupitia vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, na magazeti. Pia, michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, na mpira wa pete na riadha ni mbinu bora za kuhamasisha jamii kudumisha amani ya nchi yetu. Michezo hii hujenga uhusiano mwema na kukuza urafiki miongoni mwa watu na pia kati ya jamii moja na nyingine. Matumizi bora ya mitandao ya kijamii kama “Facebook”, “WhatsApp”, “Instagram” na “Twitter” ni njia nyingine ya kutoa elimu ya kudumisha amani. LY Njia hizi huwezesha jamii kushirikiana na hata kujadiliana namna ya kudumisha amani katika jamii. Aidha, njia hizi husaidia kusambaza habari kwa haraka na hivyo huweza kusaidia kuepusha uvunjifu wa amani katika jamii. N O Pia, nchi yetu inaweza kutumia tarehe 21 Septemba, siku ambayo imetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa siku ya amani duniani ili kuelimisha na kuhamasisha jamii kudumisha amani nchini. Katika siku hii, masuala mbalimbali kuhusu SE udumishaji wa amani yanaweza kuwasilishwa na kujadiliwa kupitia mikutano, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. U Hali kadhalika, madhehebu ya dini yana fursa kubwa katika kudumisha amani ya nchi kwa kutumia mahubiri na mawaidha kwa waumini wao. Waumini huhubiriwa umuhimu wa amani kama msingi mkuu unaowawezesha kuabudu E kwa uhuru na utulivu. Kwa kutumia mahubiri na mawaidha, upendo na amani huimarika miongoni mwa wanajamii. N LI Umuhimu wa kudumisha amani katika jamii Amani ina umuhimu mkubwa katika ustawi wa jamii. Jamii yenye amani huwa N na nafasi ya kushiriki vizuri katika shughuli za uzalishaji mali. Shughuli hizi za uzalishaji mali huongeza kipato na kuondoa umaskini kwa wananchi. Kwa O hiyo amani ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi. Amani inapotawala katika jamii huwapa wanajamii fursa ya kutumia rasilimali R wanazomiliki kwa manufaa ya wote. Mahali penye amani watu huweza FO kujenga makazi ya kudumu, kusomesha watoto na kujitafutia kipato kwa njia mbalimbali. Jamii yenye amani hujenga umoja na mshikamano. Amani huifanya jamii kushirikiana na kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. 26 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 26 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY DO Angalia Kielelezo namba NOTjibu 1, kisha DUPLICATE maswali yanayofuata. LY N O SE U Kielelezo namba 1: Vitendo vya kuhamasisha amani katika jamii Zoezi la 1 E 1. Kwa kutumia Kielelezo namba 1, eleza kwa kifupi uhusiano N uliopo kati ya amani na nchi ya uchumi wa viwanda. LI 2. Kwa kutumia Kielelezo namba 1 fafanua ujumbe unaosema “usawa wa jinsia na amani”. N 3. Je, umejifunza nini katika Kielelezo namba 1? O R Kazi ya kufanya namba 1 Fanya uchunguzi katika jamii inayokuzunguka, kisha bainisha mbinu FO wanazotumia kulinda amani. Wasilisha darasani kwa majadiliano zaidi. 27 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 27 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY Kuthamini utu DO NOT DUPLICATE Kuthamini utu ni kuwajali na kuwathamini binadamu kwa kuhakikisha kuwa hawapati mateso yoyote yasiyo ya lazima. Binadamu anayethamini utu huwa na upendo, huheshimu watu wengine na kutowavunjia haki na heshima yao. Umuhimu wa kuthamini utu Katika maisha ya kila siku na katika mazingira yetu tuna watu wa aina na jinsi tofauti wanaotuzunguka. Watu hawa, wanahitaji matendo ya utu, hususan kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wao. LY Binadamu akioneshwa upendo wa kweli kwa kuthamini mahitaji yake muhimu kama vile chakula, malazi, mavazi na elimu, naye hujenga tabia ya upendo na kuheshimu utu wa watu wengine. Hali hii humwezesha kukuza mshikamano na N watu wengine kwa sababu atajiona anathaminiwa katika jamii inayomzunguka O na anapendwa kutokana na kutendewa matendo yenye kuthamini utu. Haki za binadamu ndiyo msingi wa kujenga na kudumisha utu wa binadamu. SE Haki za binadamu zinaweza kugawanywa kwenye makundi manne ambayo ni haki za kisiasa, kijamii, kiuchumi, na kiutamaduni. Udumishaji wa haki za binadamu husaidia kuthamini utu kwa sababu haki za binadamu ndiyo U mwongozo wa jinsi ya kuhusiana na binadamu wengine tofauti na jinsi tunavyohusiana na viumbe wengine. E Aidha, mtu anapothaminiwa utu wake katika jamii humfanya ajione ana wajibu mkubwa wa kutimiza katika jamii yake. Hali hii humfanya ajitoe kwa moyo wake N wote kuitumikia, kuitetea na kuilinda jamii yake na pia kuiletea maendeleo. LI Hali kadhalika, mtu akiheshimiwa katika jamii humfanya aishi kwa amani na utulivu katika jamii yake. N Vitendo vya kuthamini utu O Mwanzo wa kuthamini utu ni kujiheshimu. Kujiheshimu ni hali ya kutambua thamani ya utu ambayo humwezesha mtu kuvaa mavazi ya heshima na kuepuka vitendo viovu. Vitendo hivyo viovu ni kama vile ukahaba, utumiaji R mihadarati na lugha ya matusi. Aidha, kila binadamu hana budi kuheshimu FO binadamu wenzake kwa kuthamini nafasi zao katika jamii. Nafasi hizo ni kama vile; wazazi, walezi, viongozi na watu wa umri mdogo na mkubwa. Watoto na vijana wanapaswa kuwaheshimu wazazi na watu wengine wenye umri unaowazidi kwa kuwasalimia na kuonesha utii kwao. Kuonesha na kutunza 28 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 28 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY heshima ni kitendo chaDO NOT utu. kuthamini DUPLICATE Kupenda watu wengine na kuwajali katika hali zao, pia ni kitendo cha kuonesha utu. Kuonesha matendo kama vile kuwavusha barabara watoto wadogo katika barabara zenye msongamano wa magari na kuwapokea mizigo wazee ni vitendo vya upendo. Pia, kusaidia wazazi na majirani katika kazi za nyumbani na kuwahudumia wagonjwa na wenye uhitaji wa aina mbalimbali ni vitendo vinavyoonesha upendo na kujali utu. Hivyo, kutoa misaada ni kitendo kimojawapo cha kuthamini utu. LY Aidha, mtu anayezingatia bidii na maadili katika kazi zake, atakuwa akidumisha utu wake katika jamii anamoishi au kufanya kazi. Kazi ni kipimo cha utu. Tendo jingine muhimu la kuthamini utu ni kujisitiri na kuwasitiri wengine kwa N kauli njema au kutunza siri za watu wengine. Kwa mfano, kama ndugu au O rafiki yako anakabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii na asingependa taarifa hiyo ijulikane kwa wengine, huna budi kumsaidia kwa kutunza siri hiyo. Zoezi la 2 SE 1. Eleza kwanini kutoa misaada kwa watu au taasisi ni kitendo cha U kuthamini utu. 2. Je, kwa namna gani kuishi kwa kuzingatia maadili kunawezesha kuthamini utu? E 3. Kwanini haki za binadamu ni nguzo muhimu katika kuthamini N utu? LI 4. Eleza njia tano zinazoonesha kuthamini utu katika jamii. N Kazi ya kufanya namba 2 O Kwa kushirikiana na wanafunzi wenzako katika kikundi, fanya majadiliano kuhusu vitendo vya kuthamini utu katika jamii unamoishi. Kisha, R andika majibu mliyopata katika daftari lako la mazoezi. FO Uhuru na umoja wa Taifa letu Uhuru wa taifa ni hali ya taifa moja kutotawaliwa na mtu au nchi nyingine kiuchumi, kisiasa na kijamii. Taifa lililo huru huwa na uwezo wa kufanya uamuzi wake bila kuingiliwa na taifa jingine. Uhuru wa taifa ni muhimu sana 29 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 29 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY katika kutekeleza mipangoDO NOTmfupi ya muda DUPLICATE na muda mrefu katika masuala ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii. Tanzania ni Taifa huru linaloundwa na muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar zilizoungana mwaka 1964. Umoja wa kitaifa ni hali ya watu wa taifa moja kuwa na ushirikiano na mshikamano katika mambo mbalimbali kama vile kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa. Pia, umoja wa kitaifa ni hali ya wananchi kuwa na msimamo mmoja kuhusu jambo au mambo yanayolihusu taifa lao. Umoja wa kitaifa ni nguzo muhimu kwani taifa lisilo na umoja hushindwa kujiletea maendeleo kutokana na kukosekana kwa nguvu ya pamoja katika kutekeleza mipango yake ya LY maendeleo. Tanzania ni kati ya mataifa yenye umoja imara barani Afrika kwa kuwa lina mshikamano imara na limeweza kupata maendeleo makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. N O Ulinzi wa Taifa huhitaji umoja wa wananchi wote. Kila mwananchi ana jukumu la kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda uhuru na umoja wa Taifa letu. Umuhimu wa kulinda uhuru na umoja wa Taifa SE Nchi yenye uhuru na umoja hupata maendeleo haraka. Pia, nchi yenye uhuru U na umoja hupata faida kubwa ya kuwa na nguvu ya pamoja katika masuala ya kitaifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Aidha, uhuru na umoja hudumisha amani katika taifa, na husaidia taifa kutekeleza mipango yake E kwa mafanikio kutokana na ushiriki na uungwaji mkono wa wananchi katika malengo yanayotakiwa kufikiwa. N LI Nchi yenye uhuru na umoja hudumisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao. Nchi inapokuwa huru, inakuwa na amani na salama ndani ya mipaka N yake hivyo watu wake hupata muda wa kutekeleza mipango yao ya kiuchumi, kijamii na kisiasa bila kuwa na hofu ya kuingiliwa na yeyote. O Ushirikiano na mshikamano wa wananchi husaidia kufanya kazi kwa bidii ili kuwezesha nchi istawi. Hali hii huharakisha maendeleo ya nchi kwa kuwa R kila mtu huona anastahili kuwajibika kwa ajili ya kuleta maendeleo binafsi na FO Taifa kwa ujumla. “Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu”. Vitendo vya kulinda uhuru na umoja wa Taifa Kila taifa linatakiwa kufanya jitihada kuhakikisha uhuru na umoja wake 30 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 30 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY vinalindwa. Jambo hili DO NOTkutimizwa linaweza DUPLICATEikiwa Serikali na wananchi kwa pamoja watafanya yafuatayo: (a) Kutii sheria: Kila taifa lina sheria zake kwa mujibu wa katiba, ni lazima lihakikishe watu wake wanazifuata. Utii wa sheria, kanuni na taratibu katika nchi huondoa uwezekano wa kuibuka machafuko yanayoweza kupoteza amani ya nchi na hivyo watu wake kukosa umoja wao. Wananchi wa taifa fulani wanapotii sheria, kanuni na taratibu za nchi, amani na mshikamano katika taifa hutamalaki. (b) Kulinda mipaka ya nchi: Ili nchi iweze kulinda uhuru na umoja wake ni lazima kulinda mipaka yake dhidi ya maadui kutoka nje. Maadui hawa LY ni kama wahamiaji haramu, vikundi vya kigaidi na kijasusi. Kuwapo kwa makundi haya huweza kuvuruga umoja na uhuru wa nchi. Kwa mfano, nchi ya Tanzania inasifika kwa amani na umoja wa kitaifa kutokana na N kazi kubwa ya kulinda mipaka yake dhidi ya maadui. Jeshi la Wananchi O wa Tanzania limepewa jukumu la kulinda mipaka ya nchi yetu. Hata hivyo, kila mwananchi ana wajibu wa kulinda mipaka ya nchi yetu na mali zake. (c) Kuheshimu haki za binadamu: Taifa linaloheshimu haki za binadamu ni SE rahisi kulinda uhuru na umoja wa watu wake. Hii ni kwa sababu haki za binadamu zinapolindwa husaidia watu kuishi katika taifa lao kwa uhuru na amani. Kuheshimu haki za binadamu husaidia wananchi kujivunia na U kuipenda nchi yao. Vilevile, huondoa migogoro inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuharibu umoja wa kitaifa. Wananchi wasipopata haki zao, huichukia nchi yao na hii ni hatari kwa uhuru na umoja wa kitaifa. E (d) Kukemea vitendo viovu kwa wakati: Ili nchi iweze kuendelea kulinda uhuru na umoja wa taifa lake ni muhimu kuwa na tabia ya kukemea N vitendo viovu kama wizi, unyang’anyi, rushwa, uchochezi wa kisiasa na LI kikabila na vitendo vya kutotii sheria. Serikali haina budi kupiga marufuku vitendo hivyo na kuvikemea mara kwa mara ili kuhakikisha amani na N mshikamano miongoni mwa wananchi vinadumishwa. (e) Kujenga uhusiano mwema na mataifa mengine: Uhusiano mzuri na O mataifa mengine huwezesha nchi kuwa na mipango ya pamoja katika uzalishaji mali, huduma za kijamii kama elimu na afya, usafirishaji, ulinzi na usalama. Kwa mfano, nchi ya Tanzania na nchi nyingine zilizo R katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, zinashirikiana katika kukomesha FO matendo ya kihalifu katika nchi zao. Kama mtu atafanya uhalifu nchini Tanzania na kukimbilia nchini Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi au Sudani Kusini, bado vyombo vya usalama katika nchi hizo huendelea kumsaka mtuhumiwa na endapo atakamatwa, atarudishwa nchini ili 31 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 31 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY DOwaNOT ashitakiwe kwa mujibu DUPLICATE sheria. Zoezi la 3 1. Tofautisha dhana ya uhuru wa Taifa na umoja wa kitaifa. 2. Taja faida za kudumisha uhuru wa nchi yetu na umoja wa Taifa. 3. Ni kwa namna gani ulinzi wa mipaka ya nchi husaidia kulinda uhuru na umoja wa kitaifa? LY Kazi ya kufanya namba 3 Katika mazingira ya jamii yako, bainisha mambo mawili ambayo N yanaweza kusababisha kupoteza uhuru na umoja katika jamii yako. Andika hatua unazoweza kuchukua kudhibiti mambo hayo ili yasilete madhara zaidi. O Zoezi la 4 SE A: Andika Kweli kwa sentensi iliyo sahihi na Si Kweli kwa sentensi isiyo sahihi katika sehemu iliyoachwa wazi. U 1. Amani ni hali ya uhasama baina ya mtu na mtu au jamii na jamii nyingine._________ 2. Kutii sheria bila shuruti ni mojawapo ya vitendo vya kudumisha amani E katika jamii.______ N 3. Mitandao ya kijamii inaweza kutumika kama njia mojawapo ya kuhamasisha amani katika jamii.________ LI 4. Kuthamini utu ni hali ya kutoheshimu mtu mwingine._________ N 5. Kutenda haki ni mojawapo ya vitendo vya kuthamini utu.__________ O R B: Chagua jibu sahihi, kisha andika herufi yake kwenye kisanduku. FO 6. Lipi kati ya yafuatayo ni kitendo kisicho cha kudumisha amani katika jamii? (a) kutii sheria bila shuruti 32 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 32 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT (b) kukemea vitendo viovu DUPLICATE (c) kulinda mipaka ya nchi (d) kutotumia mitandao ya kijamii kulingana na sheria 7. Kati ya vitendo vifuatavyo kimojawapo si kitendo cha kusaidia kuhamasisha amani kwenye jamii. (a) kubishana na majirani zako (b) kutumia mitandao ya kijamii kupinga ubaguzi (c) kutumia mikutano na semina kujadili umoja LY (d) kuandaa kisamafunzo na ngonjera kuhamasisha upendo katika jamii N 8. Kujisitiri na kuwasitiri wengine vinasaidiaje jamii? (a) kuhamasisha amani katika jamii O (b) kuthamini utu (c) kutokujipenda sana (d) SE kujipenda kwanza na wengine baadaye 9. Kutenda haki husaidia kulinda uhuru na umoja wa Taifa kwa sababu U gani? (a) viongozi wa nchi hutoa maagizo (b) watu huwa na uhuru wa kufanya lolote walipendalo E (c) raia huwa huru kufanya ugaidi N (d) wananchi huipenda nchi yao LI 10. Jukumu la kulinda uhuru na umoja wa Taifa letu ni jukumu la nani? (a) usalama wa Taifa tu N (b) polisi tu O (c) idara ya uhamiaji tu (d) kila mwananchi R FO 33 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 33 30/07/2021 20:42 FOR ONLINE USE ONLY DO Sehemu C: Oanisha kipengele kutoka NOT DUPLICATE A na maneno yaliyopo Sehemu B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika nafasi uliyopewa. Sehemu A Jibu Sehemu B 11. Utu (a) kuwa na nguvu ya pamoja katika masuala 12. Umuhimu ya kitaifa wa amani (b) hali ya kuwa na tabia zisizo za kibinadamu katika jamii (c) huduma za uhuru wa mawazo 13. Kuwa na (d) Taifa kugawanyika umoja wa LY kitaifa (e) huchochea maendeleo katika jamii 14. Kuheshimu (f) kitendo cha kuthamini utu N haki za (g) vitendo vya kulinda uhuru na umoja wa binadamu Taifa O 15. Kutoa (h) hali ya kuwa na tabia nzuri ya kibinadamu msaada kwa watu au taasisi SE U Msamiati E Adhimu kitu chenye ubora wa pekee, chenye maana na umuhimu N Mihadarati dawa za kulevya Shuruti lazima, bila hiyari LI N O R FO 34 URAIA DARASA LA 7 FINAL.indd 34 30/07/2021 20:42