Summary

This document is a syllabus on oral literature for education in Swahili.

Full Transcript

FASIHI KWA UJUMLA Fasihi: Ni sanaa inayotumia lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa. Ni sanaa kwa sababu huumbwa kwa lugha katika hali ya kuvutia na kuweka madoido ya kila namna ili iweze kuvutia wasomaji au wasimuliaji wake, lengo lake kuu ni kufikisha ujumbe kwa jamii. SANAA Ni u...

FASIHI KWA UJUMLA Fasihi: Ni sanaa inayotumia lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa. Ni sanaa kwa sababu huumbwa kwa lugha katika hali ya kuvutia na kuweka madoido ya kila namna ili iweze kuvutia wasomaji au wasimuliaji wake, lengo lake kuu ni kufikisha ujumbe kwa jamii. SANAA Ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisia zinazomgusa kwa kutoa kielelezo chenye maana. Hivyo unaona kazi za sanaa katika nyanja mbalimbali kama vile: – – Utarizi – Fasihi – Ushonaji – Muziki – Ususi – Ufumaji uchoraji DHIMA ZA FASIHI (i) Kusisimua 1 (ii) Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii (iii) Kudumisha na kuendeleza lugha (iv) Kuelimisha jamii (a) KUSISIMUA Hujikita zaidi katika mpangilio wa maneno lugha ya picha mandhari, tamathali au semi Mfano: – Ndugu yetu ametutupa mkono (amefariki) Sentensi inajaribu kutuliza uchungu na hivyo kuleta faraja. (b) Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii Fasihi huhifadhi na kutunza mila na desturi za fani na pia huweza kurithisha mila hizo kutoka kizazi kimoja hadi kingine. (c) Kudumisha na kuendeleza lugha Kwa kadri lugha inavyotumiwa na watumizi, maneno yalivyobuniwa na kuenezwa zamani, leo yanatumiwa na watunzi wa mashairi, kwaya , nyimbo n.k (d) Kuelimisha jamii Fasihi hukosoa, huonya na kurekebisha jamii hueleza waziwazi wale wanaotenda kinyume na matakwa ya jamii, inabidi kukemea na kuonyana kwa kutumia methali, nahau Mfano: – Asiyesikia la mkuu huvunjika guu Hii inatoa tahadhari AINA ZA FASIHI 2 Kuna aina mbili (2) za fasihi (a) Fasihi andishi (b) Fasihi simulizi 1. FASIHI SIMULIZI Ni fasihi ambayo hutumia masimulizi ya mdomo kufikisha ujumbe wake kwa jamii. Ni fasihi ambayo ni kongwe na ilianza tangu binadamu alipoanza kuishi duniani. FASIHI SIMULIZI INA TANZU NNE NAZO NI (i) Hadithi (ii) Semi (iii) Ushairi (iv) Maigizo 2. FASIHI ANDISHI Ni fasihi ambayo hutumia maandishi ili kufikisha ujumbe kwa jamii Fasihi Andishi: 1. Hadithi Fupi - hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine 2. Riwaya - hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee 3. Tamthilia - mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi 4. Ushairi* - mashairi yaliyoandikwa 3 Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi ni kwamba Fasihi Simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au matendo ilhali Fasihi Andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Tanbihi:Ushairi ni kipera cha nyimbo lakini pia mashairi yanaweza kuwa chini ya Fasihi Andishi, ikiwa yamechapishwa TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI NA FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI Huwasilishwa na fanani kwa njia ya Huwasilishwa kwa maandishi kwa njia ya 1 masimulizi au mdomo maandishi Huifadhiwa kichwani na kusambazwa Huifadhiwa kwa maandishi na 2 na mdomo au mazungumzo kusambazwa kwa maandishi Hairuhusu mabadiliko ya papohapo kazi 3 Huruhusu mabadiliko ya papo kwa papo ikishaandikwa haibadiliki hadi toleo jingine Ina tanzu nne kama vile – Hadithi – Ina tanzu tatu kama vile – Ushairi – 4 Semi – Sanaa za maonesho Tamthilia – Riwaya maigizo Hadhira yake ni watu wale katika jamii Hadhira yake ni watu wale wanaojua 5. – Watoto – Wazee – Wasomi kusoma na kuandika Ina umri mdogo imekuwepo baada ya 6 Inaumri mkubwa ugunduzi wa maandishi 4 Si rahisi kusahauliwa baadhi ya vipengele 7 Ni rahisi kusahau baadhi ya vipengele kwani imehifadhiwa kwa maandishi. Mara nyingi muundo wake ni wa 8 Muundo wake ni wa moja kwa moja mchangamano unaruhusu urejeshi Huenda na wakati na mabadiliko ya Haiendi na wakati kwa sababu 9 matukio katika jamii ikishaandikwa haiwezi kubadilishwa. Umuhimu wa Fasihi Katila Jamii: Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira. Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii. Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho. Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha. Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika. Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko nk. 5 TANZU ZA FASIHI SIMULIZI Fasihi simulizi hujitokeza katika tanzu kuu nne, ambazo ni hadithi, semi, ushairi, na maigizo. Tanzu hizi zinaweza kuoneshwa katika mchoro ufuatao na vipera vyake HADITHI Ni tungo za fasihi simulizi zitumiazo lugha ya ujazo na maongezi ya kila siku. Masimulizi huwa ni mafupi yaliyopangwa katika mtiririko unaokamilisha visa. VIPERA VYA HADITHI (i) Ngano (ii) Tarihi (iii) Vigano (iv) Soga NGANO Hizi ni hadithi zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu kuelezea au kuonya. 6 TARIHI Ni hadithi ambazo husimulia kuhusu matukio ya kihistoria, matukio hayo yanaweza kuwa ya kweli au ya kubuni. VIGANO Ni hadithi fupi zinazoelezea makosa au uovu wa watu fulani na kueleza maadili yanayofaa. Vigano hutumia methali kama msingi wa maadili yake. SOGA Ni hadithi fupi za kuchekesha na kukejeli. Wahusika wa soga ni watu wa kubuni. Soga husema ukweli unaohimiza lakini ukweli huo hujenga vichekesho ili kupunguza makali. USHAIRI Ushairi katika fasihi simulizi ni fungu linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo ya sauti kwa utaratibu maalumu VIPERA VYA USHAIRI (i) Mashairi (ii) Utenzi (iii) Nyimbo (iv) Ngonjera MASHAIRI Ni tungo zenye mpangilio maalumu wa silabi na lugha ya mkato. UTENZI 7 Ni tungo ndefu ya kimasimulizi au kimawaidha utenzi kutofautiana na ushauri kwa kuwa na mistari mifupimifupi isiyozidi mizani. NYIMBO Ni tungo zenye mpangilio maalumu wa maneno na mahadhi yaani hupenda kuimbwa na kuambatana na ala za muziki au sanaa. NGONJERA Zina muundo wa mashahiri ya kimapokeo na huwa katika muundo wa mazungumzo baina ya watu wawili au makundi ya watu wanaolumbana na mwishowe kufikia mwafaka/ suluhisho. SEMI Ni tungo za fasihi simulizi ambazo ni fupi na zenye kutumia lugha ya picha. VIPERA VYA SEMI (i) Methali (ii) Mafumbo (iii) Nahau (iv) Vitendawili METHALI Ni misemo ambayo hutoa hekima na busara kwa kuundwa kwa mpangilio wa pande mbili za fikra Mfano: – – Kidole kimoja hakivunji chawa – Haba na haba hujaza kibaba 8 MAFUMBO Ni kauli zinazoeleza maana waziwazi na kutumia maficho Mfano:- – Hakamatiki hashikiki (moshi) – Uzalendo umemshinda ( umeshindwa kuvumilia) KITENDAWILI Ni usemi uliofumbwa hutolewa kwa hadhira, ufumbuliwe, kitendawili kufanya kazi ya kumfikisha msikilizaji. Mfano: – Uzi mwembamba umefunga dume (usingizi) NAHAU Ni kauli zilizojengwa kwa picha kwa kutumia maneno ya kawaida lakini zinatoa maana isiyo ya kawaida. Mfano: – – Amepata jiko (ameoa) – Ana mkono mrefu (mwizi) – Ana mkono wa birika (mchoyo) – Amevaa miwani (amelewa) MAIGIZO SANAA ZA MAONYESHO: Ni masimulizi yenye utendaji ambayo huonesha mambo yaliyotokea, yatakayotokea lengo ni kufikisha ujumbe. 9 VIPERA VYAKE NI:- (i) Michezo ya kuigiza (ii) Majigambo (iii) Ngonjera (iv) Vichekesho MICHEZO YA KUIGIZA Ni maigizo marafu ya visa vinavyowakilisha maisha ya jamii fulani. Michezo mingine huafiki na mingine hulaani mambo yasiyofaa, michezo ya watoto wadogo pia huwasaidia kujifunza maadili ya jamii hiyo. MAJIGAMBO Ni maigizo ya kujitapa /kujigamba kutokana na kuweza kufanya jambo la kishujaa au lisilo la kawaida. Mtambaji husimulia na kutenda akionyesha jinsi alivyofanya jambo lile. Mfano: – Askari aliyerudi vitani,mtu aliyemuua simba n.k NGONJERA Ni maigizo ya kutumia mashairi, huwa kuna pande mbili unapinga na unaelewa jambo na mwisho kufikia muafaka. VICHEKESHO Ni maigizo mafupi ya kufurahisha hadhira Mfano: – – Mizengwe 10 – Original komedi – Vituko show FANI NA MAUDHUI Kazi ya fasihi lazima iwe na fani na maudhui, vipengele hivi ni sura za falsafa moja si rahisi kuzitenganisha fani imo ndani ya maudhui. FANI Ni umbo la nje la kazi ya fasihi MAUDHUI Ni jambo analosema muandishi katika kazi yake ya fasihi VIPENGELE VYA FANI (i) Matumizi ya lugha (ii) Mtindo (iii) Muundo (iv) Mandhari au mazingira (v) Wahusika (vi) Jina la kitabu. MATUMIZI YA LUGHA Msanii hutoa lugha kwa mpangilio maalumu wa maneno, tamathali za semi hutumiwa kwa upekee kulingana na mahitaji ya kazi hiyo. MTINDO 11 Hii ni tabia ya pekee mtunzi katika simulizi au uandishi mtindo kutofautiana hali ya mtunzi na mtunzi. MADHARI Ni sura ya mahali mazingira ambapo kazi ya fasihi husika WAHUSIKA Ni watu, miti au viumbe hai vinavyowakilisha watendaji katika kuonyesha sifa za ndani na nje. VIPENGELE VYA MAUDHUI Kuna vipengele (5) vya maudhui navyo ni (i) Dhamira (ii) Ujumbe (iii) Falsafa (iv) Migogoro (v) Mafunzo DHAMIRA Ni lengo la mtunzi wa kazi za fasihi. Mtunzi anaweza kutoa dhamira kuu na kujenga dhamira ndogondogo dhamira huweza kukosoa. UJUMBE Ni funzo analotoa mtunzi katika kazi ya fasihi kulingana na dhamira alizotoa FALSAFA 12 Ni mawazo makuu ya mtunzi kuhusu maisha. Ni imani ya maandishi kuhusu maisha. MIGOGORO Ni hali ya kutoelewa na baina ya pande mbili au zaidi. MAFUNZO Ni mafunzo makuu ya mtunzi kuhusu maisha.wakati mwingine hadhira inaweza kupata mafunzo mabaya au mazuri kwa wahusika wakazi hiyo. UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI Maana; Uhakiki ni kazi au kitendo cha kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi. au Uhakiki ni sayansi maalum ya kuchambua kazi ya sanaa kwa undani na kuona ubora wa kazi ya fasihi kwa kutumia vipengele vya fani na maudhui na kuangalia uwiano na uhusiano wake na jamii. UMUHIMU WA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI: 1. Kuchambua na kuweka wazi fumbo ambalo litapatikana na kazi ya fasihi. 2. Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi. 3. Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora. 4. Kumuelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila dira ya muhakikiki (mhakiki ni mwalimu wa jamii) 5. Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi. 13 6. Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji. 7. Kutafuta na kuweka sawa nadharia ya vitabu teule. KUFAFANUA VIGEZO VYA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI. 1. Ukweli wa mambo yanayoelezwa. 2. Uhalisikaji wa watu, mazingira na matukio katika jamii. 3. Umuhimu wa kazi ya fasihi kwa jamii inayohusika lazima ufikiriwe. UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI KATIKA FANI. Wahusika Mandhari Mtindo FASIHI SIMULIZI: Maana ya fasihi simulizi na tanzu zake kwa mujibu wa wataalam mbalimbali Maana ya fasihi simulizi: Fasihi simulizi ni sanaa ya matumizi ya lugha ya kubuni inayosambazwa kwa mdomo kwa njia ya kuimbwa, kughaniwa, kuigizwa, kusimuliwa, kuumbwa, kufumba au kutegeana mafumbo na vitendawili (Syambo na Mazrui, 1992:2) katika King’ei na Kisozi, (2005:7). Mulokozi, (1996:24) anaeleza kuwa fasihi simulizi ni fasihi iliyotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Ni tukio linalofungamana na muktadha (mazingira) fulani wa kijamii au wa kutawaliwa na mwingiliano wa mambo kadhaa wa kadhaa kama vile, fanani, hadhira, fani, na maudhui yaliyokisudiwa na mwasilishaji. 14 TUKI, (2004) fasihi simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile, hadithi, ngoma na vitendawili. Aidha, fasihi simulizi ni ile ambayo inapitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kupitia neno la mdomo (Ngure, 2003:1). Kwa ujumla, tunaweza kusema kuwa fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo ambapo kuna uambatanishaji wa utendaji katika uwasilishaji huo. Fanani na hadhira huonana ana kwa ana jambo ambalo huwafanya hadhira kushiriki katika baadhi ya utendaji. Kwa mfano, kuimba, kucheza, au kupiga makofi na vigelegele. Tanzu za fasihi simulizi Wamitila, (2003) anadai kuwa tanzu ni istilahi inayotumika kuelezea au kurejelea aina za kazi mbalimbali za kifasihi. Hivyo basi, kutokana na maana ya tanzu iliyotolewa na Wamitila, (2003) tunaweza kusema kuwa tanzu ni istilahi ya kifasihi inayotumika kumaanisha matawi au mafungu katika kazi za fasihi. Tanzu za fasihi simulizi zimeainishwa kwa namna tofauti tofauti kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali kama ifuatavvyo: Wamitila, (2008) katika uainishaji wake wa fasihi simulizi anazigawa tanzu za fasihi simulizi katika makundi yafuatayo: Simulizi au hadithi; huu ni utngo wenye visa vya kubuni au halisi unaowasilishwa kwa lugha ya nathari kwa kusudi la kuburudisha, kukuza maadili na kuunganisha jamii. Katika usimuliaji wa hadithi fanani huwa mfaraguzi ili asiwachoshe watazamaji wake kwa kuingiza utendaji unaowashirikisha watazamaji wake. Maigizo; ni sanaa inayotumia utendaji kuiga tabia au matendo ya watu wengine au viumbe wengine ili kuburudisha au kutoa ujumbe kwa jamii. Maigizo ni sanaa inayopatikana katika makabila mengi ya kiafrika na huambatana na utambaji wa ngoma. Kwa mfano, jando na unyago, malumabno ya watani na vichekesho. Ushairi (nyimbo); ni sanaa ya uimbaji inayoambatana na mdundo wa ngoma au mziki ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Katika fasihi simulizi nyimbo 15 huambatana na mdundo wa ngoma na mara nyingi nyimbo hizi huwa na mkutdha kulingana na ujumbe uliolengwa. Hivyo basi, tunapata nyimbo za ndoa/arusi, jando/tohara, hodiya, kimai, nyimbo za mazishi, nyimbo za kidini, nyimbo za kizalendo na nyimbo na mapenzi. Semi; ni mafungu ya maneno ambayo hutumiwa kuleta maana nyingine badala ya maneno halisi ya maneno yaliyotumika. Katika fasihi ya Kiswahili semi hujumuisha nahau, misemo na methali. Kwa mfano, tukisema mtu amegonga mwamba hatumanishi kwamba amepiga jiwe kubwa kwa mkono au kwa kifaa chochote, bali tunamanisha kwamba ameshindwa kuendelea katika jambo fulani. Mazrui & Syambo, (1992) wanasema kuwa fasihi simulizi ina tanzu zake ambazo ni tofauti na zile za fasihi andishi ingawa kuna baadhi amabazo zinafanana na zile za fasihi andishi. Fasihi simulizi ina tanzu kuu nne ambazo tunaziainisha kama ifuatavyo: Ngano au hadithi; ni tungo yoyote ya kubuni inayosimuliwa kwa lugha ya nathari. Katika fasihi ya Kiswahili ngano ni za aina nyingi lakini zote huanza kwa njia inayofuata mtindo huu: Msimulizi : Paukwa! Msikilizaji : Pakawa! Msimulizi : hapo zamani za kale palitokea… Nyimbo au mashairi; kuna nyimbo za aina nyingi katika fasihi ya Kiswahili lakini zinazokusudiwa hapa ni zile zilizotungwa kwa mdomo (bila maandishi) na kusambazwa kwa mdomo. Nyimbo za aina hii zimeenea katika maisha ya Kiswahili na huwafata tangu wanapozaliwa mpaka kufa kwao. Nyimbo hizi kwa kawaida huwa zinafungamana na ngoma au michezo fulani na mara nyingine huimbwa pamoja na mziki kwa mfano, nyimbo za sherehe, nyimbo za watoto, nyimbo za taarabu na bembezi. Methali; hii ni misemo mifupi yenye hekima fulani ndani yake. Methali hudhihirisha mkusanyiko wa mafunzo waliopata watu wa vizazi vingi vya jumuia fulani katika maisha yao. Methali hutumiwa sana katika mazungumzo ya kawaida ya waswahili na ni sehemu moja muhimu katika fasihi simulizi ya 16 Kiswahili. Methali nyingi za Kiswahili huwa na mdundo maalumu wa kishairi na mara nyingine huwa na vina. Vitendawili; ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi lisili wasi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huuliza swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitaji kufkiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa na neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalumu kulingana na jamii yake. Katika fasihi simulizi vitendawili huwalenga watoto ili kuchochea fikra na kuwazoeaza mazingira yanayowazunguka. Mulokozi katika makala yake ya tanzu za fasihi simulizi iliyo katika jarida la Mulika Na 21 (1989) amezigawa tanzu na vipera vya fasihi simulizi kwa kutumia vigezo viwili ambavyo ni: 1. Umbile: na tabia ya kazi inayohusika; katika kigezo hiki, Mulokozi ameangalia vipengele vya ndani vinavyounda sanaa hiyo na kuipa mwelekeo au mwenendo. Baadhi ya vipengele hivyo vya ndani ni namna lugha inavyotumika kishairi, kinathari, kimafumbo, kiwingo au kughani, muundo wa fani hiyo na wahusika. 2. Muktadha; ambapo amezingatia kuwa fasihi simulizi ni tukio, hivyo huambatana na mwingiliano wa mambo matatu ambayo ni muktadha, watu na mahali. Mwingiliano huu ndio unaotupa muktadha na muktadha ndio unaoamua fani fulani ya fasihi simulizi ichukue umbo lipi, iwasilishwe vipi kwa hadhira kwenye wakati na mahali hapo. Hivyo hadithi inaweza kugeuzwa wimbo, utendi unaweza kuwa hadithi na wimbo unaweza kugeuzwa ghani au usemi kutegemea muktadha unaohusika. Utata katika uainishaji wa tanzu za fasihi simulizi Vigezo vya uainishaji; baadhi ya wataalamu wametumia vigezo vya uainishajia mbavyo vinatofautina kati ya mwandishi mmoja na mwingine. Lakini pia watalaamu weingine kama kama vile Wamitila, (2008), mazrui & Syambo, (1992) hawajaonesha vigezo vyovyote vya uanishaji wa tanzu za fasihi simulizi jambo ambalo linaleta utata katika uainishaji kwani ni vigumu kubaini ni yupi uainishaji wake upo sahihi. 17 Utofauti wa Idadi katika tanzu zinazoainishwa; uainishaji wa tanzu hizi unatofautiana katika idadi wanazoainshisha wataalamu mbalimbali. Kwa mfano, Mulokozi katika jarida la Mulika Na 21 (1989) anadai kuna tanzu sita (6), Balisidya, Matteru(1987) anainisha tanzu tatu (3), Wamitila, (2008) na Okpewho, (1992) wanaainisha tanzu nne (4) za fasihi simulizi. Hivyo kutofautina kwa idadi za tanzu zinazoainishwa na watalaamu mbalimbali kunazua utata kwani ni vigumu kuhitimisha kuwa ni nani yupo sahihi. Kuingiliana kwa tanzu; katika uainishaji wa watalamu mbalimbali baadhi ya tanzu zinaingiliana ingawa hutofautiana katika vigezo vya uainishaji wao na wengine kukosa vigezo kabisa. Hivyo basi kuingiliana kwa tanzu hizo huweza kuleta utata. Kwa mfano, Okpewho, (1992) ameainisha utanzu wa ngojera ambao unaingia katika utanzu wa ushairi kama ilivyoainishwa na Wamitila, (2008), Mulokozi, (1989). Lakini pia utanzu wa semi umeonekana katika kila uainishaji ingawa kuna utofati unaojitokeza katika uainishaji wao. Utofauti wa isitlahi za uainishaji; baadhi ya wataalamu wametofautina katika isitilahi za uainishaji ingawa hurejelea utanzu mmoja au dhana moja. Kwa mfano, Balisidya & Matteru, (1987) anatumia istlahi nathari, Wamitila, (2008) ametumia hadithi, Okpewho, (1992) na Mulokozi, (1989) ametumia istilahi masimulizi. Tukichunguza istalahi hizo, tunapata dhana moja tu inayorejelewa na kuleta utata katika uainishaji. Tanzu za fasihi simulizi hubadilika badilika kifani, kimaumbo na hata kimaudhui; baadhi ya tanzu za fasihi na vipera vyake huweza kubadilika kulingana na wakati. Kwa mfano utanzu wa hadithi katika kipindi cha sasa huwasilishwa tofauti na ulivyowasilishwa zamani, hivyo basi hukosa uhalithia wa hadithi kama utanzu wa fasihi simulizi kitendo ambacho waainshaji hushindwa kutengeza kigezo cha kuainisha utanzu huu. Hivyo basi, tunahitimisha kwa kusema kuwa, fasihi simulizi kama fasihi zingine ina dhima muhimu katika jamii. Dhima za fasihi simulizi ni kama vile kuelimisha jamii, kufundisha jamii, kutabirii na kutoa mwelekeo wa jamii, kuhifadhi historia ya jamii na kuonya jamii. Pia kupitia fasihi simulizi wasimuliaji hukuza ubunifu wao kwa kutongoa masimulizi au hadithi mbalimbali. Fasihi simulizi ni chanzo kikubwa cha fasihi andishi kwani karibu vipengee au tanzu zote za fasihi andishi zimetokana na fasihi simulizi. Kwa mfano, riwaya chanzo chake ni hadithi, tamthiliya hutokana na sanaa za maonesho, semi mbalimbali za fasihi simulizi hupatikana katika fasihi 18 andishi. Utanzu wa ushairi umetokana na ushairi simulizi ambao zamani ulikuwa ukiwasilishwa kwa uimbaji au kughani fasihi simulizi hukuza upeo wa kufikiri na ubunifu kwa hadhira kupitia elimu inayopatikana kupitia masimulizi mbalimbali. Fasihi ya Kiafrika: Fasihi ya Kiafrika inamaanisha maandiko kuhusu na kutoka Afrika. Kama Yusufu George anavyodokeza katika ukurasa wa kwanza wa sura yake kuhusu Fasihi ya Afrika katika kitabu "Understanding Contemporary Africa", ' wakati mtizamo wa fasihi ya Ulaya kwa ujumla inahusu herufi zilizoandikwa, dhana ya Afrika inahusisha pia fasihi simulizi. Kama anavyoendelea kuandika, wakati maoni ya Ulaya kuhusu fasihi yalisisitiza mgawanyo wa sanaa na maudhui, mwamko wa Afrika unajumuisha: "Fasihi" inaweza pia kuashiria matumizi ya maneno kisanaa kwa ajili ya sanaa pekee. Bila kukana jukumu muhimu la somo la sanaa katika Afrika, tunapaswa kukumbuka kwamba, tangu jadi, Waafrika huwa hawatenganishi sanaa na kufundisha. Badala ya kuandika au kuimba kwa sababu ya uzuri uliomo, waandishi wa Afrika, kwa kufuata fasihi simulizi, hutumia uzuri kusaidia kuwasiliana ukweli na taarifa muhimu na jamii. Hakika, kitu huchukuliwa kizuri kwa sababu ya ukweli kinachoonyesha na jamii kinachosaidia kujenga. Maandiko ya kale Misri ya Kale ulikuwa miongoni mwa tamaduni za kale zaidi za Kiafrika zenye desturi ya kuandika, ambao baadhi ya maandishi yake yaliyotumia picha na alama kuashiria kitu au jambo huishi mpaka leo. Kazi kama vile Kitabu cha Wafu cha Misri kawaida hutumiwa na wasomi kama rejeleo la msingi la imani ya kidini ya Misri ya kale na sherehe. Maandiko ya Kinubi yanakubalika lakini kwa wakati huu hayasomeki. Awali yaliandikwa kwa kutumia picha na alama na hatimaye kwa kutumia alfabeti yenye herufi 23, kutafsiri kumekuwa kugumu. Fasihi simulizi: 19 Fasihi simulizi inaweza kuwa katika nathari au ushairi. Mara nyingi, nathari huwa hadithi au historia na inaweza kujumuisha hekaya zenye wahusika bandia. Wasimulizi katika Afrika wakati mwingine hutumia mbinu ya maswali-na-majibu kusimulia hadithi zao. Mashairi, ambayo mara nyingi huimbwa, hujumuisha: masimulizi ya visa, aya ya shughuli, aya ya kidini, mashairi ya kusifu watawala na watu wengine maarufu. Waimbaji wa sifa husimulia hadithi zao kwa kuimba. Nyimbo za mapendo, za kazi, za watoto, misemo, mithali na vitendawili pia husomwa au huimbwa. Kwa ujumla fasihi simulizi huundwa kwa tanzu kuu nne (4) ambazo ni: Hadithi/Nathari, Ushairi/Nudhumu, Semi na sanaa za maigizo. Na kila utanzu una vipera vyake. Fasihi kabla ya Ukoloni: Mifano ya fasihi ya Kiafrika kabla ya ukoloni ni mingi. Fasihi simulizi ya Afrika ya magharibi inajumuisha visa vya Sundiata vilivyotungwa katika Mali ya kale, Visa vya zamani vya Dinga kutoka Dola la kale la Ghana. Nchini Ethiopia, iliyoandika awali kwa herufi za Ge'ez ni Kebra Negast au Kitabu cha Wafalme. Aina moja maarufu ya ngano za kiafrika ni hadithi za "ulaghai", ambapo wanyama wadogo hutumia akili zao kushinda mapambano na wanyama wakubwa. Mifano wa wanyama laghai ni pamoja na Anansi, buibui katika ngano za Waashanti kutoka Ghana; Ijàpá, kobe katika ngano za Wayoruba kutoka Nigeria; na Sungura, ambaye hupatikana katika ngano za Afrika ya Mashariki na Afrika ya kati. Kazi nyingine zilizoandikwa ni tele, yaani katika Afrika kaskazini, kanda ya Sahel ya Afrika magharibi na pwani ya Kiswahili. Kutoka Timbuktu peke yake, kuna nakala 300,000 au zaidi zilizowekwa katika maktaba mbalimbali na mikusanyiko ya binafsi, hasa zilizoandikwa kwa Kiarabu, lakini baadhi yazo katika lugha za wenyeji (yaani Peul na Songhai) Nyingi ziliandikiwa katika Chuo Kikuu maarufu cha Timbuktu. Kazi hizi zinaongelea mada 20 nyingi, ambazo ni pamoja na Unajimu, Ushairi, Sheria, Historia, Imani, Siasa na Falsafa miongoni mwa nyingine. Fasihi ya Kiswahili vilevile, imehamasishwa na mafundisho ya Kiislamu lakini ilikua katika mazingira ya kienyeji. Kati ya vipande vya fasihi ya Kiswahili vinavyojulikana na vya kitambo sana kimojawapo ni Utendi wa Tambuka au "Hadithi ya Tambuka." Katika nyakati za Kiislamu, Waafrika wa Magharibi kama vile ibn Khaldun walitia fora sana katika fasihi ya Kiarabu. Afrika Kaskazini ya kale ilinufaisha Vyuo vikuu kama vile vya Fez na Cairo, kwa kiasi kikubwa mno cha maandiko ili kuongeza yao. Fasihi ya Kiafrika wakati wa ukoloni: Kazi nzuri za Kiafrika zinazojulikana Ulaya kutoka kipindi cha ukoloni na kile cha biashara ya utumwa ni za masimulizi ya utumwa, kama vile The Interesting Narrative of the Life of Olaudah Equiano (1789) cha Olaudah Equiano. Katika kipindi cha ukoloni, Waafrika walioathiriwa na lugha za Ulaya walianza kuandika katika lugha hizo. Mwaka 1911, Yusufu Efraimu Casely- Hayford (ajulikanaye pia kama Ekra-Agiman) kutoka Pwani ya Dhahabu (sasa Ghana) alichapisha ile ambayo pengine ni riwaya ya kwanza ya Kiafrika kuandikwa kwa Kimombo, Ethiopia Unbound: Studies in Race Emancipation Ingawa kazi hii iligusia hadithi na utetezi wa kisiasa, uchapishaji na kupitiwa upya na wanahabari wa Ulaya kulimaanisha wakati muhimu katika fasihi ya Kiafrika. Katika kipindi hiki, tamthilia za Kiafrika zilianza kuibuka. Herbert Isaka Ernest Dhlomo wa Afrika ya Kusini alichapisha tamthilia ya kwanza ya Kiafrika kwa Kiingereza katika mwaka wa 1935. Mwaka 1962, Ngugi wa Thiong'o kutoka Kenya aliandika mchezo wa kuigiza wa kwanza wa Afrika ya Mashariki, The Black Hermit, hadithi iliyohadhari "ukabila" (ubaguzi kati ya makabila ya Afrika). Fasihi ya Afrika mwishoni mwa kipindi cha ukoloni (kati ya mwisho wa Vita Vikuu vya Kwanza Vya Dunia na uhuru) iliendelea kuonesha mandhari ya ukombozi, uhuru, na (walau kati ya Waafrika kwenye maeneo yaliyotawaliwa 21 na Ufaransa) kutambua weusi wa Waafrika. Mmoja wa viongozi wa harakati za kutambua weusi, mshairi na hatimaye Rais wa Senegal, Sédar Léopold Senghor, alichapisha mkusanyo wa kwanza wa mashairi ya lugha ya Kifaransa yaliyoandikwa na Waafrika mwaka 1948, Anthologie de la Nouvelle poésie nègre et malgache de langue Française, akishirikisha utangulizi kutoka kwa mwandishi wa Kifaransa Jean-Paul Sartre. Si kwamba waandishi wa fasihi ya Afrika wakati huo walikuwa mbali na masuala waliyoyakabili. Wengi, kwa hakika, waliteswa kwa undani na pia kwa kuelekezwa: akilaaniwa kwa kuyaweka kando majukumu yake ya kisanaa ili kushiriki kikamilifu katika mapambano, Christopher Okigbo aliuawa katika vita vya Biafra dhidi ya wanaharakati wa Nigeria katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1960; Mongane Wally Serote aliwekwa kizuizini kati ya miaka 1969 na 1970 chini ya sheria ya Afrika Kusini juu ya Ugaidi ya mwaka 1967, na hatimaye kutolewa bila hata kujibu mashtaka; mwananchi mwenzake Arthur Norje alijiuamjini London mwaka 1970; Jack Mapanje wa Malawi aliwekwa kizuizini bila kesi au tuhuma kwa sababu ya matamko aliyotoa katika baa ya chuo kikuu; na, mwaka 1995, Ken saro-Wiwa alikufa kwa kutiwa kitanzi na serikali ya wanajeshi ya Nigeria. Fasihi ya Afrika baada ya ukoloni: Kwa ukombozi na kuongezeka kwa kusoma na kuandika kwani mataifa mengi ya Afrika yalipata uhuru wao katika miaka ya 1950 na hasa miaka ya 1960, fasihi ya Afrika imekua kwa kasi kwa wingi na kwa umaarufu, kwa kazi nyingi za Afrika kuonekana katika mitaala ya elimu ya Ulaya na katika orodha ya "vitabu bora" vilivyoandikwa mwishoni mwa karne ya 20. Waandishi wa Afrika katika kipindi hiki waliandika katika lugha za Ulaya (hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno) na pia lugha za jadi za Afrika. Ali A. Mazrui na wengine hutaja migogoro saba kama mandhari: Farakano kati ya Afrika iliyopita na iliyopo, kati ya Utamaduni na Usasa, kati ya wazawa na wageni, kati ya kujijali na kujali jamii, kati ya Ujamaa na Ubepari, kati ya maendeleo na kujitegemea na kati ya Uafrika na ubinadamu. Mandhari mengine katika kipindi hiki ni pamoja na matatizo ya kijamii kama vile ufisadi, tofauti za kiuchumi kati ya nchi ambazo zimepata uhuru majuzi, 22 na haki na majukumu ya wanawake. Waandishi wa kike wamewakilishwa vyema katika fasihi ya Afrika iliyochapishwa kuliko walivyokuwa kabla ya uhuru. Mwaka 1986, Wole Soyinka alikuwa mwandishi wa Afrika wa kwanza baada ya uhuru kushinda Tuzo la Nobel katika fasihi, ingawa Camus Albert, mzaliwa wa Algeria, alipokea tuzo hilo katika mwaka 1957. Tuzo la Noma, lilianza mwaka wa 1980, hupatiwa kwa kazi bora ya mwaka katika fasihi ya Afrika. 23

Use Quizgecko on...
Browser
Browser